1. Bado safari ni ndefu,wasafiri tusichoke. Na tusiwe wadhaifu,twendeni hadi tufike. Tusiwe na hofu,mwenye nafsi ziwatoke. Huu ndio mwanzo wake, sio mwisho wa safari 2. Twendeni tusonge mbele, twendeni tusianguke Mwaona mlima ule,pale ndipo mwisho wake Tupande chake kilele,bendera tuitunike Huu ndio mwanzo wako,sio mwisho wa safari 3. Ni njia yenye misitu,na mirefu miti yake lmejaa Wanyama mwitu,kila mmoja na pake Na wakionapo kitu,na lazima wakishike Huu ndio mwanzo wake,sio mwisho wa safari 4. Wenzangu na waimiza haya ana myatilie Elimu ndio mwangaza,na mola hatujalie